KAZE AJIPANGA KIVITA ZAIDI / KUMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA KIBABE.

 Baada ya kutua jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Rukwa ambako juzi walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa raundi ya 18 ligi kuu ya Vodacom, kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema hesabu zake ni kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Tangu atue pale mitaa ya Jangwani mwezi Oktoba, Kaze ameiongoza Yanga katika michezo 13, akishinda michezo nane na kutoka sare michezo mitano

Kocha huyo wa zamani Academy ya FC Barcelona amesema, anatambua mzunguuko wa pili utakuwa utakuwa na ushindani mkali hivyo nao wamejipanga kupambana kuhakikisha wanatimiza lengo lao

"Tunashukuru, tumefunga mwaka 2020 tukiwa tunaongoza ligi. Tunajua mzunguuko wa pili utakuwa mgumu lakini nasi tutapambana kuhakikisha tunatimiza malengo yetu"

"Lengo kuu ni kuchukua ubingwa, ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu," alisema Kaze muda mfupi baada ya kutua jijini Dar jana

Yanga inaelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo

Wananchi watashuka dimbani Januari 05 kuikabili Jamhuri Fc

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form