Tetesi za Soka Ulaya Leo Alhamisi 22.04.2021: Mourinho, Mbappe, Kane, Bailly, Lingard, Aguero, Johnstone


Jose Mourinho alitimuliwa Tottenham Hotspur Jumatatu

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Jose Mourinho, ambaye alipigwa kalamu kama kocha wa Tottenham Hotspur Jumatatu, amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwa mkufunzi wa Celtic. (Sun)

Valencia pia wamehusishwa na kocha huyo wa Ureno, wakati mmiliki wa klabu hiyo Peter Lim anajiandaa kumtimua kocha wa sasa Javi Gracia kumleta Mourinho aliye na emri wa miaka 58. (Todofichajes - in Spanish)

Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers, 48, amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Tottenham. (Talksport)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anahofia huenda hadi wachezaji 10 wangeondoka klabu hiyo msimu huu wa joto kama hangelimfuta Mourinho. Levy alikuwa na wasiwasi zaidi kumhusu Muingereza Harry Kane, 27, na Dele Alli, 25, pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Eurosport)

Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji ambao wangeondoka klabu hiyo msimu huu wa joto kama Mourinho asingeondolewa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona wamempatia ofa ya mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32. Muargentina huyo yuko huru kuondoka kwa uhamisho wa bure mkataba wake utakapomalizika uwanja wa Etihad msimu huu wa joto. (TyC Sports - in Spanish)

Real Betis wanataka kumsajili mlinzi wa Ivory Coast Eric Bailly,27, kutoka Manchester United msimu huu. (Sun)

Aston Villa huenda wakamnunua kiungo wa kati mshambulizi wa Manchester United na England Jesse Lingard msimu huu wa joto. West Ham United pia wanapania kumpatia mkataba wa kudumu Lingard mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa akiwachezea kwa mkopo tangu mwezi Januari. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Beki wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car, 24, ana matumaini Liverpool itafufua azma ya kumtaka ajiunge nao hasa wakati huu ambapo klabu yake iko tayari kumuachilia. (RMC Sport, via Team Talk)

West Bromwich Albion wamejitolea kusalia na kipa wao Sam Johnstone,28, katika uga wa Hawthorns. Manchester United na West Ham pia wanamtaka mchezaji huyo raia wa Uingereza. (Express and Star)

Newcastle United wanamtaka beki wa Benfica wa chini ya miaka 21- Mreno Nuno Tavares. (Record, via Sport Witness)

Mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Brighton & Hove Albion kuhusu mpango wa kumpatia mkataba wa kudumu kipa wa Australia Mat Ryan,29, ambaye kwa sasa yuko klabu hiyo kwa mkopo. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, ameanza mkakati wa kuhamia Madrid. Mshambulizi huyo wa Ufaransa bado hajakubali kutia saini mkataba mpya PSG na kwa muda mrefu amehusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid. (Goal)

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form