YOCUBA APEWA MAPUMZIKO YANGA

 Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Sogne amepewa mapumziko ili aweze kupona majeraha aliyopata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc

Yacouba anatibiwa majeraha ya mbavu aliyopata kwenye mchezo huo. Nyota huyo aliyefunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao, hakuweza kucheza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons juzi

Wakati Yanga ikitarajiwa kwenda visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, Yacouba huenda akabaki jijini Dar es salaam kukamilisha matibabu yake

Yacouba amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga katika mechi za hivi karibuni akifunga au kusababisha bao kwenye mechi nne za mwisho alizoshiriki kabla ya kuumia

Raia huyo wa Burkina Faso amewafunga midomo wakosoaji waliokuwa wakiponda usajili wake baada ya kuanza kufanya vizuri katika kila mchezo alioshuka uwanjani

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form