ZIDANE: "HAZARD ANAHITAJI MUDA KUREJESHA MAKALI YAKE"


 


Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Zidane ameonesha imani yake kwa straika wa klabu hiyo Eden Hazard kwamba atarudi kwenye makali yake ila anahitaji kupewa muda wa kutosha.

Hazard ambae tangu ajiunge na klabu hiyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara alirejea jana katika mchezo wao ambao walitoa sare ya 1-1 na klabu ya Elche.

"Hazardi anahitaji muda, ingawa ni taratibu ila naimani atarejea kwenye makali yake na kuanza michezo yote" ZIDANE.

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Elche 

"Nadhani tulipata nafasi nyingi sana katika mchezo huu ambazo zingetuwezesha kupata goli la pili katika kipindi cha pili ila tulikosa umakini wa kuzitumia"  ZIDANE

Bao la Real madrid katika mchezo huu lilifungwa na L. Modric  dakika ya 20' huku bao la Elche likifungwa kwa mkwaju wa Penalt dakika ya 52'.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form