LEWANDOWSK HAPOI / ATUPIA TENA GOLI MBILI

 



NYOTA wa Bayern Munich, Robert Lewandowski na Manuel Neuer jana walipewa heshima kwa ushindi wao wa tuzo za FIFA, huku timu yao ikiichapa Bayer Leverkusen 2-1 katika mchezo wa Bundesliga Uwanja wa BayArena.
Bayer Leverkusen ilitangulia kwa bao la Patrik Schick dakika ya 14 kabla ya Lewandowski kusawazisha dakika ya 43 na kufunga la pili dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo, Bayern Munich inafikisha pointi 30 na kuendelea kuongoza Bundesliga kwa pointi mbili zaidi ya Bayer Leverkusen baada ya wote kucheza mechi 13.

Hadi sasa lewandowsk amefunga magoli 17 katika michezo 13 aliyocheza katika Bundesliga.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form