MUARGENTINA Lionel Messi jana amefikia rekodi ya Pele ya kufunga mabao 643 katika klabu moja baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 45, Barcelona ikitoa sare ya 2-2 na Valencia Uwanja wa Camp Nou.
Messi amefunga mabao hayo katika mechi 747 Barcelona huku pia akitoa pasi za mabao 282, wakati Pele alifunga katika mechi 656 akiwa na Santos ya kwao, Brazil.
Bao lingine la Barcelona jana alifunga Ronald Araujo dakika ya 52, wakati ya Valencia yalifungwa na Mouctar Diakhaby dakika ya 29 na Maximiliano Gomez dakika ya 69.
Bao lingine la Barcelona jana alifunga Ronald Araujo dakika ya 52, wakati ya Valencia yalifungwa na Mouctar Diakhaby dakika ya 29 na Maximiliano Gomez dakika ya 69.
Kwa matokeo hayo, Barcelona imefikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 13, ikizidiwa pointi nane na vinara Atletico Madrid ambao pia wana mechi moja mkononi.
Katika kipindi chote hicho, Messi ameiwezesha Barcelona kutwaa mataji 24, yakiwemo 10 ya LaLiga na manne ya Ligi ya Mabingwa na pia ametwaa tuzo sita za Ballon d'Or.
Kwa upande wake, gwiji wa Brazil, Pele amecheza miaka 18 Santos, kabla ya kuhamia New York Cosmos ya Marekani.