Katika mpira wa miguu imezoeleka kwamba Makipa ni wachezaji wa pande moja uwanjani wakijihusisha na kulinda gol.
Rogerio Ceni alikuwa kipa wa Brazil ambae aliiwakilisha timu yake ya Taifa katika ushindi wa kombe la dunia la mwak 2002. Ceni alizaliwa januari 22 mwaka 1973 nchini Brazil, alifanya maajabu ya kufunga mabao mengi zaidi ukilinganisha na washambuliaji au wachezaji wengine waliokuwa wanacheza nafasi za mbele kwa wakati huo. Alikuwa kipa bora na hata aliwakilisha nchi yakeya Brazil kwenye Makombe mawili ya Dunia. Alikuwa mzuri sana katika upigaji wa vipande vipande (Setpieces) Kama vile faulo na penati.
Katika karia yake aliyodumu kwa miongo miwili na nusu, Ceni alifunga mabao 131, mbali na magoli ya mipira ya adhabu ceni aliwahi pia kufunga goli la kawaida. Hayo ni mabao 60 zaidi ya kipa wa pili mwenye utajiri mkubwa wa historia, Jose Luis Chilavert. Kuweka mtazamo huu wa kushangaza, Ryan Giggs, mchezaji anayeshambulia, amefunga mabao 111 tu katika kipindi hicho hicho ambacho Ceni alianza kuchukua vipande (Setpieces) kwa timu yake.
Baada ya kustaafu Ceni alifanya kazi kama Meneja wa klabu ya Sao Paulo na na kufanikiwa kushinda jumla ya mataji 20 ikiwemo kombe la dunia la vilabu. Kwa sasa Ceni ni meneja wa klabu ya Flamengo.
Mpaka sasa ndo goalkeeper mwenye mabao mengi zaidi duniani. Hakika rekodi hii ni kubwa na ya jabu sana katika historia ya soka na makipa bora duniani.