TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMA MOSI 24.04.2021: KONATE, MESSI, RONALDO, KING, WILOCK WAHUSISHWA NA USAJILI.


Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi

Rais wa Barcelona Joan Laporta anashughulikia mkataba wa miaka mitatu kumpa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi katika jaribio la kumshawishi mchezaji huyo wa miaka 33 abaki klabuni humo. (ESPN)

Mshambuliaji wa Everton raia wa Norway Josh King anafanya mazungumzo na Galatasaray ya Uturuki na mchezaji huyo wa miaka 29 anaonekana kuwa na nia ya kuondoka klabu hiyo msimu huu wa joto. (Football Insider)

Mshambuliai wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo,

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliai wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, anatamani kurudi Manchester United msimu huu wa joto. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Arsenal wana wasiwasi kuwa wanaweza kumpoteza mchezaji kutoka Norway Martin Odegaard, 22, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Real Madrid, kwa sababu ya kujitoa kwenye Ligi Kuu ya Ulaya.(Sun)

Beki wa Ufaransa Ibrahima Konate

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Beki wa Ufaransa Ibrahima Konate

Liverpool wamekubaliana masharti ya kibinafsi na RB Leipzig kwa beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 21, ambaye kifungu cha kuachiliwa kwake kutoka kwa klabu hiyo ya Bundesliga ni £ 34m. (Fabrizio Romano on Twitter)

Kocha wa muda wa Sheffield United Paul Heckingbottom anatarajia kiungo wa kati wa Norway 23 Sander Berge kubaki na klabu hiyo iliyoshuka daraja, licha ya nia kutoka kwa Arsenal na Tottenham kumsajili . (Sheffield Star)

Barcelona wanajaribu kumrudisha tena kiungo wa Ufaransa Kays Ruiz-Atil klabuni

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Barcelona wanajaribu kumrudisha tena kiungo wa Ufaransa Kays Ruiz-Atil klabuni

Barcelona wanajaribu kumrudisha tena kiungo wa Ufaransa Kays Ruiz-Atil klabuni huku mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 18 huko Paris St-Germain ukimalizika mwishoni mwa msimu.(Mundo Deportivo - in Spanish)

Mlinda lango chaguo la tatu wa Manchester United Lee Grant, mwenye umri wa miaka 38, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto na Muingereza huyo akihisi kuwa klabu hiyo imekiuka makubaliano ya kumpa mktaba mpya (Mail)

Mchezaji wa Mali Yves Bissouma

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Mali Yves Bissouma anasemekana kuwa mchezaji anayeweza kuimarika

Meneja wa Brighton Graham Potter anasema kiungo wa Mali Yves Bissouma anaweza kuimarika na the Seagulls, ambao hawapaswi "kuogopa" nia ya timu nyingine zinazotaka huduma zake kama vile liverpool (Express)

Afisa mkuu Mtendaji wa manchester United anayemaliza muda wake Ed Woodward anatarajiwa kuchagua mrithi wake kabla ya kuondoka klabuni hapo. Manchester Evening News)

Joe Willock
Maelezo ya picha,

Newcastle itahitaji kuilipa Arsenal mamilioni ya pauni kumsajiri Joe Willock

Newcastle itahitaji kuilipa Arsenal takribani pauni milioni 20 ili kumsajili kiungo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 Joe Willock kwa mkataba wa kudumu. (Telegraph - subscription required)

Mmiliki wa Leeds Andrea Radrizzani anatumai meneja Marcelo Bielsa ataongeza kandarasi yake huko Elland Road kabla ya mwisho wa msimu huu. (L'Equipe - in French)

Mlinzi wa Manchester City mreno Pedro Porro

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mlinzi wa Manchester City mreno Pedro Porro

Kiungo wa kati wa Aston Villa, Carney Chukwuemeka, 17, anafuatwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia ikiwamo Manchester United na Manchester City. (Guardian)

Mlinzi wa Manchester City mreno Pedro Porro, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Sporting Lisbon, anaivutia Real Madrid inayomezea mate huduma zake. (AS - in Spanish)

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form