REAL MADRID WAJA KIVINGINE WAPANDA KILELENI KISHUJAA

 



MABAO ya Lucas Vazquez dakika ya sita na Marco Asensio dakika ya 53 jana yameipa  Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa LaLiga Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid.
Kwa ushindi huo,  Real Madrid inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda kileleni mwa La Liga ikiwazidi pointi moja tu wapinzani wao wa Jiji, Atletico Madrid ambao hata hivyo wamecheza mechi 14.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form