MAANDALIZI YA CHAN YAPAMBA MOTO / TAIFA STAR YAANZA KUPASHA



BEKI mpya wa timu ya soka taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiwa mazoezini leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Januari 10 na 13.

Kiungo Feisal Salum akijiandaa na mechi hizo ni mechi maalum za Taifa Stars kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),  zitakazofanyika nchini Cameroon kuanzia Januari 16 hadi Februari 7, mwaka huu.


Kiungo Farid Mussa akijiandaa na CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na Zambia, Guinea na Namibia.

Kundi linaundwa na Cameroon, Mali, Burkina Faso na Zimbabwe, Kundi B; Libya, DRC, Kongo na Niger na Kundi C lina mabingwa watetezi Morocco, Rwanda, Uganda na Togo.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form