ALIYETOA HUKUMU KESIY MORRISON JELA MIAKA MIWILI

 Taarifa iliyotamba sana jana ni kufungiwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Elias Mwanjala ambaye Serikali imemfungia kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kujitwalia madaraka kinyume na Sheria

Mwanjala alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoani Mbeya na amevuliwa vyeo na nyadhifa zake zote katika michezo kwa kipindi cha miaka miwili

Wengi wanamkumbuka Mwanjala kwa hukumu yake katika shauri la Mkataba wa Bernard Morrison na Yanga akibatilisha mkataba huo akidai kubaini mapungufu

Yanga ilipinga hukumu hiyo na kulipeleka shauri Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS)

Jaji wa kusikiliza shauri hilo amepatikana na litaanza kusikilizwa kuanzia Januari 12. Uongozi wa Yanga una matumaini makubwa kuwa wataipata haki yao huko CAS

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form