KOEMAN: BARCELONA INAHITAJI STRAIKA MPYA

Kocha mkuu wa klabu ya Barcelona Koeman amedai kuwa klabu yake ya Barcelona inauhitaji wa straika mpya, Koeman amesema hayo baada ya timu yake kuonesha ubutu wa hali ya juu katika eneo la ushambuliaji wa jana juma pili.

Katika mchezo huo ambao Barcelona iliibuka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Huesca, Barcelona ilifanikiwa kupiga mashuti 20 na kati hayo mashuti 7 saba tu ndo yalilenga goli la mpinzani huku wakifunga goli moja pekeyake.

 Hivyo hali hiyo imemfanya kocha wa klabu hiyo kuona kuwa klabu yake inauhitaji wa straika mpya katika dirisha dogo la usajili mwezi huu ili kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Barcelona kwa sasa inashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu Hispania wakiwa na pwenti 28 baada ya kucheza m ichezo 16, wapo nyuma ya vinara wa ligi hiyo Atletco madrid kwa pwenti 10, Atleco madrid wamecheza michezo 15 pekee na wana jumla ya pwenti 38.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form