TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA: MANCHESTER UNITED MBIONI KUFANYA DILI LA MABADILISHANO NA JUVENTUS.

 

Tetesi za soka barani Ulaya zinaonesha kuwa klabu ya manchester united ipo kwenye mazungumzo ya dili la mabadilishano kati ya nyota wa klabu hizo mbili Poul Pogba na christino Ronaldo.

Ni muda mrefu sasa kiungo wa manchester united Poul Pogba amekuwa hana furaha ndani ya kikosi hicho kutokana na kutokufanya vizuri katika mfululizo wa michezo mbalimbali pamoja na kufanya makosa mengi hali iliyofanya kocha mkuu wa klabu hiyo kutompanga katika kikosi cha kwanza kwa michezo mingi.

Upande wa Juventus na Christino Ronaldo, inasemekana kwamba klabu hiyo inalenga kutua mzigo wa mshahara wa nyota huyo mkubwa wa dunia, hii ni kutokana na madhara makubwa ya kiuchumi yaliyosababishwa na ugonjwa wa Korona na kupelekea pato la klabu hiyo kushuka. Hivyo inasemekana kwamba juventus wapo tayari kumuachia nyota huyo aondoke wakati wowote klabuni hapo.

Ronaldo (35) ambae kwa msimu huu ameonekana kuonesha kiwango cha hali ya juu katika ligi kuu nchini Italia akiwa amefunga jumla ya mabao 16 katika jumla ya michezo 14 aliyoicheza katika mashindano yote.

Mbali na manchester united, Ronaldo pia anahusishwa na kujiunga na klabu ya PSG ambayo msimu huu imeonekana kutokufanya vizuri katika ligi ya Ufaransa.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form