RATIBA KAMILI YA LIGI YA EUROPA BARANI ULAYA / MANCHEZTER UNITED KUWASHA MOTO DHIDI YA REAL SOCIEDAD

 



Manchester United itamenyana na vinara wa LaLiga, Real Sociedad katika hatua ya 32 UEFA Europa League
 


TIMU ya Manchester United itamenyana na vinara wa LaLiga, Real Sociedad katika hatua ya 32 UEFA Europa League.
Baada ya kuangukia kwenye michuano hiyo kufuatia kutolewa katika Ligi ya Mabingwa, kocha Ole Gunnar Solskjaer atakabiliwa na matihani mwingine mgumu mbele ya timu inayoongoza kwa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya Hispania kwa sasa.
Arsenal nayo imepangiwa mpinzani mgumu katika Hatua hii, ambayo ni Benfica ya Ureno huo ukiwa mtihani mwingine kwa kocha Mikel Arteta kufuatia matokeo mabaya mfululizo msimu huu.
Kocha maarufu, Mreno Jose Mourinho kidogo hatakuwa na kazi ngumu baada ya Tottenham Hotspur kupangiwa Wolfsberger ya Austria.
Mechi ya Tottenha itachezwa Saa 24 kabla ya nyingine Jumatano ya Februari 24, kwa sababu Arsena watakuwa wana mechi pia, hivyo Jiji la London haliwezi kuwa na michezo miwili ya Europa League wakati mmoja.
Leicester City ni timu nyingine iliyopata mpinzani mwepesi kidogo, kwani itamenyana na Slavia Prague.

RATIBA KAMILI

Wolfsberg vs Tottenham Hotspur

Dynamo Kyiv vs Club Brugge

Real Sociedad vs Manchester United

Benfica vs Arsenal

Crvena Zvezda vs AC Milan

Royal Antwerp vs Rangers

Slavia Prague vs Leicester City

Salzburg vs Villarreal

Braga vs Roma

Krasnodar vs Dinamo Zagreb

Young Boys vs Bayer Leverkusen

Molde vs Hoffenheim

Granada vs Napoli

Maccabi Tel-Aviv vs Shakhtar Donetsk

Lille vs Ajax

Olympiacos vs PSV Eindhoven

Mechi za kwanza zitachezwa Alhamisi ya Februari 18; marudiano Alhamisi ya Februari 25

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form