MANCHESTER UNITED WAIGARAGAZA WOLVES.

Baada ya kutoa sare ya magoli mawili na klabu ya Leicester wiki iliyopita, klabu ya mabchester united jana wamefanikiwa kupata ushindi muhimu katika dimba lao la nyumbani ndidi ya klabu ya Wolves.

Manchester united walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri katika mchezo wa jana dhidi ya wolves, bao ambalo lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 93 baada ya kupata pasi ndefu (Assist) kutoka kwa Bruno Fernandes.

Ushindi huo umekuwa muhimu kwa klabu hiyo kwani umeiwezesha kupanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Wingereza baada ya kucheza michozo 15  na kukusanya jumla ya pwent 30 huku wakiwa na mchezo mmoja wa kiporo mkononi.

Manchester united wanatarajia kucheza mhezo wao wa kiporo siku ya ijumaa dhidi ya klabu ya Aston Villa. Aston villa wamekuwa na msimu mzuri baada ya kushinda baadhi ya klabu kubwa kwenye ligi hiyo kama vile Liverpool ambao walifungwa mabao saba, Aston Villa wamekusanya jumla ya pwenti 26 msimu huu wakiwa wamecheza mihezo 14 tu na kushikilia nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form