KOCHA WA BARCELONA SETIEN ATHIBITISHA KUWA MESSI YUPO FITI KUCHEZA DAKIKA 90'.



Kocha wa klabu ya Barcelona Quique Setien amethibitisha kuwa nyota wa klabu hiyo Lionel Messi yupo tayari kucheza dakika tisini katika mchezo utakaopigwa leo juma mosi Mei 13 dhidi ya Molloraca, mchezo utakao anza majira ya saa tano usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Klabu ya Barcelona inacheza mchezo wake wa kwanza wa Laliga baada ya mapumziko marefu ya Corona.huku wakiongoza ligi ya hispania kwa pwent mbili mbele ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid ambao watacheza siku ya juma pili Mei 14 dhidi ya Eiber.

Aidha Setien amesema kuwa Suarez atakua fiti kucheza mechi hiyo lakini hana uhakika kama atacheza dakika zote za mchezo. Suarezi ambae ana jumla ya magoli 14 katika michuano yote, hajahusika kwenye kikosi cha klabu hiyo tangu mwezi Januari kutokana na majeraha.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form