MIAMBA KUREJEA DIMBANI LEO / TAZAMA RATIBA YA EPL LEO JUMA MOSI

 

JUMA MOSI FEBRUARI 6, 2021

Klabu ta Arsenal Baada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya wolves kwa mabao mawili kwa moja leo wanarejea tena dimbani kupambana na Aston Villa ambao nao walipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya West ham kwa mabao matatu kwa  moja.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa ni mchezo wa kuvutia sana huku vilabu vyote vikijitahidi kujikwamua kurud kwenye nafasi za juu. Katika mchezo wao wa mwisho uliochezwa mwezi Novemba mwaka jana Arsenal walipoteza kwa mabao matatu kwa sifuri.

Aston Villa vs Arsenal (15:00)

Burnley vs Brighton (18:00)

Newcastle vs Southampton (18:00)

Fulham vs West Ham (20:30)

Man Utd vs Everton (23:00)

Manchezster United nao leo wanarejea uwanjani baada ya kupata ushindi mzito wa mabao tisa kwa sifuri dhidi ya Southampton wiki hii, ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mwisho wa ligi ulioikutanisha Man utd na Everton Mwezi Novemba mwaka jana, Man utd waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa kwa moja ugenini.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form