PINDUZI CUP: NI VITA YANGA VS NAMUNGO LEO

Baada ya kulazimishwa matokeo ya bila ya kufungana kwenye mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri Fc, leo Yanga inatupa karata yake ya pili kwa kuikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Amaan kuanzia saa mbili na robo usiku

Huu ni mchezo muhimu kwa kikosi cha kocha Cedric Kaze, kwani kama vinara hao wa ligi kuu watakosa ushindi, wanaweza kujikuta wakiyaaga mashindano hayo mapema

Hivyo ni mchezo ambao Kaze hatarajiwi kuanza na kikosi cha majaribio kama alivyofanya mchezo wa kwanza dhidi ya Jamhuri

Namungo ni moja ya timu zenye ushindani msimu huu, tayari imeshakutana na Yanga kwenye ligi na timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewashukuru mashabiki visiwani Zanzibar kwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kwanza, akiwataka leo wajitokeze kwa wingi zaidi kushuhudia kandanda safi litakaloambatana na ushindi

Matokeo ya ushindi kwa Yanga yatawahakikishia kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form