MESSI AFIKIA REKODI YA GWIJI WA SOKA PELE , TAZAMA UJUMBE WA PELE KWA MESSI BAADA YA KUFIKIA REKODI HIYO.


 Klabu ya Barcelona jana ilikuwa na mchezo dhidi ya Valencia mchezo ambao uliisha kwa matokeo ya sare ya magoli mawili, miongoni mwa magoli hayo goli moja lilifungwa na Staa wa klabu hiyo Lionel Messi dakika ya 45, goli ambalo lilimuwezesha Messi kufikia rekodi iliyowekwa na Gwiji wa soka dunianin Pele ya kufungha jumla ya mabao 643 ndani ya klabu moja.

UJUMBE WA PELE KWA MESSI

"Moyo wako unapofurika upendo, ni ngumu kubadili njia yako. Mimi kama wewe najua raha ya kuvaa jezi moja kila siku.

Najua kuwa hakuna kitu bora kama unapojisikia upo nyumbani, Hongera kwa rekodi yako ya kihistoria Lionel.

Lakini juu ya yote hongera kwa kazi yako kubwa huko Barcelona"

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form