Kufuatia maagizo yaliytolewa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA jinsi ya kupambana na changamoto ya ugonjwa wa Corona, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limefanya mabadiuko mbalimbali katika uendeshaji wa ligi hiyo. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo;
Moja, shirikisho limetoa ruksa kuongezwa kwa mabadiliko ya wachezaji uwanjanji kutoka wachezaji watatu kama ilivyokuwa imezoeleka hadi kufikia wachezaji watano katiaka mchezo mmoja.
Pili, shirikisho hilo limefanya pia mabadiliko jkatika kanuni ya maswala ya usajili ambapo wachezaji amabao mikataba yao ilikua inaisha mwezi Mei wakati ligi ilipotarajiwa kuisha, kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona wachezaji hao watakiwa kutumikia vilabu vyao hadi mwezi Julai tarehe 31 ambapo ligi hiyo inatarajia kumalizika.
Aidha TFF pia wamesema kuwa dirisha la usajili litafunguliwa rasmi mwezi Agosti tarehe 1 na kufungwa tarehe 30 mwezi Agosti.
Tags
SPORTS NEWS