VITA YASIMBA NA YANGA YAHAMISHWA KWA MARA NYINGINE.

Jana Bodi ya Ligi ilitangaza ratiba ya mechi za mzunguuko wa pili kuanzia raundi ya 19 mpaka raundi ya 34

Miongoni mwa mabadiliko yaliyofanyika, ni kuusogeza mbele mchezo wa pili wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopaswa kupigwa Februari 20, 2021

Kwa mara nyingine,  Bodi imeshindwa kuacha mchezo huo uchezwe kwenye tarehe waliyoipanga awali. Mechi sasa itachezwa May 08

Oktoba 18 ilikuwa tarehe ambayo mchezo wa duru ya kwanza ulipaswa kupigwa lakini ukasogezwa mbele mpaka Novemba 07

Wakati huo ilielezwa kuwa baadhi ya wachezaji (wa kigeni) wangechelewa kujiunga na timu zao kutoka majukumu ya timu za Taifa

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form